Na Timothy Lugembe ,
Mwanakwetusports.
Aliyekuwa mlinzi wa kati wa klabu ya Arsenal na pia mchezaji wa timu ya taifa ya Ghana, Thomas Partey, anakabiliwa na wakati mgumu baada ya kufikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka matano ya ubakaji pamoja na shtaka moja la unyanyasaji wa kingono, kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Jeshi la Polisi London.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na mamlaka za Uingereza, makosa hayo yanadaiwa kutokea kati ya mwaka 2021 hadi 2022, yakihusisha wanawake watatu tofauti, Polisi wamesema Partey anakabiliwa na mashtaka yafuatayo:
-Mashtaka mawili ya ubakaji dhidi ya mwanamke wa kwanza,
-Mashtaka matatu ya ubakaji dhidi ya mwanamke wa pili,
-Na shtaka moja la unyanyasaji wa kingono dhidi ya mwanamke wa tatu.
Hata hivyo, upande wa utetezi kupitia wakili wake umejitokeza na kukanusha vikali tuhuma hizo, ukisisitiza kuwa Partey anakataa mashtaka yote na anakaribisha kwa mikono miwili fursa ya kujisafisha mahakamani, huku akisisitiza kuwa ukweli utadhihirika.
Sio mara ya kwanza kwa wachezaji wakubwa kujikuta kwenye mkumbo wa tuhuma kama hizi. Mason Greenwood, aliyewahi kuichezea Manchester United, Benjamin Mendy wa zamani wa Manchester City na pia Antony anayekipiga sasa na Real Betis, wote waliwahi kukumbwa na shutuma za aina hiyo.
Partey anatarajiwa kufika tena mahakamani tarehe 5 Agosti 2025, ambapo ataendelea kujibu mashitaka yanayomkabili.
Kwa upande mwingine, kumeibuka mjadala mpana kuhusu ongezeko la visa vya unyanyasaji wa kingono vinavyowahusisha watu weusi barani Ulaya, hasa wanamichezo na wasanii, Swali linalozidi kuumiza vichwa ni Je, ni kweli watu hawa hawazielewi sheria za nchi hizo? Au kuna sababu nyingine zilizofichika nyuma ya pazia?
Ni suala linalohitaji mjadala mpana na majibu ya kina, huku haki ikitakiwa kutendeka bila upendeleo wala ubaguzi.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment