TANZIA: DIOGO JOTA NA MDOGO WAKE WAFARIKI DUNIA.

 


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Nyota wa Liverpool na timu ya taifa ya Ureno, Diogo Jota, amefariki dunia pamoja na mdogo wake André Silva kufuatia ajali mbaya ya gari iliyotokea Julai 3, 2025, katika eneo la Palacios de Sanabria, kaskazini-magharibi mwa Uhispania.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi wa barabarani wa Hispania walithibisha kuwa chanzo Cha ajali hiyo ni baada ya tairi ya gari kupasuka na kusababisha gari kuacha njia na kulipuka , vikosi vya uokoaji vilifika na havikufanikiwa kuokoa maisha ya vijana hao ambao waliokuwa tayali wamesha fariki, Miili ya marehemu ilihamishiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Zamora kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kitabibu.

Diogo Jota, ambaye alikuwa na umri wa miaka 28, alikuwa ameoa hivi karibuni na alijaliwa watoto watatu, Mdogo wake André, ambaye pia alikuwa mchezaji wa soka akikipiga katika klabu ya Penafiel ya Ureno, alikuwa akisafiri naye kuelekea Santander kwa lengo la kusafiri kurudi Uingereza, Familia ya Jota, ambayo bado iko katika hali ya mshtuko na huzuni kubwa, imetaka faragha ikihimiza vyombo vya habari na mashabiki kuheshimu kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

Wachezaji na wadau mbali mbali wameonyeshwa kuhuzunishwa kwa taarifa hizo kwa kuandika kwenye kurasa zao salamu za pole , akiwemo Cristiano Ronaldo nahodha wa Ureno, jurgen Klopp kocha wa zamani wa Liverpool, shirikisho la mpira Ureno (FPF), FIFA na vilabu vya mpira vikiendelea kutoa salamu za pole.

Na rasmi jezi namba 20 katika klabu ya Liverpool itaastafishwa kama heshima katika klabu hiyo mara ya mwisho klabu hiyo ilichukuwa ubingwa msimu ulioisha ikiwa ni kwa mara ya 20 na jezi mgongoni mwa mchezaji huyo ilikuwa namba 20 hivyo kama heshima jezi hiyo haitatumika.

Msiba huu umeacha pengo kubwa si tu kwa Liverpool na Ureno, bali kwa jumuiya nzima ya soka duniani, Jota, aliyekuwa na kipaji, nidhamu na moyo wa kujituma, alitoa mchango mkubwa katika mafanikio ya klabu na taifa lake bwana ametoa bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.



0767915473.

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments