TANZANIA NA UIBUAJI WA VIPAJI

 


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Tanzania bado inakabiliwa na changamoto kubwa katika kuibua na kukuza vipaji vya soka, hali inayotajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia Taifa kushindwa kukua kwa kasi na kuingia kwenye ushindani na nchi zilizoendelea kisoka kama vile nchi za Afrika magharibi.

Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISETA yamekuwa sehemu muhimu ya kuchambua vipaji mashuleni, lakini wadau wa soka wanasema mashindano hayo yamekosa ufuatiliaji wa kina baada ya mashindano kuisha, hivyo kufanya vipaji vilivyoibuliwa visiendelezwe ipasavyo kwasababu mashindano yanapo malizika ndipo mchakato unaishiwa hapo hakuna uendelezaji wowote unaofanyika.

Vilevile, mfumo wa elimu haujatoa msukumo wa kutosha kwa michezo kama taaluma, huku wazazi wengi wakiwa bado wanaamini mafanikio yanapatikana zaidi darasani kitu ambacho sio kweli kwani kwa ulimwengu wa hivi sasa michezo inatoa fursa zaidi katika ajira , michezo kuupuziwa katika mitaala ya elimu inatajwa kuwakatisha tamaa vijana wengi wenye ndoto ya kuwa wanamichezo wakubwa.

Wadau wa michezo wanashauri kuwepo kwa sera ya kitaifa ya soka la vijana, itakayohusisha shule, vilabu, vyuo, na TFF katika mfumo wa pamoja wa kugundua na kufuatilia vipaji vya soka kuanzia ngazi ya msingi hadi kitaifa, huku ushauri ukitolewa kuanza kwa ujenzi wa academy kwa vilabu ili vijana wapikwe , kwa sasa Tanzania academy zipo chache na zinatoa wachezaji kwa kiasi chake hapa utazitaja Azam, fountain gate, alliance na mtibwa sugar.

Kwa sasa, juhudi nyingi za kukuza vipaji zinafanywa na watu binafsi, huku vilabu vikubwa vikitegemea kusajili vipaji vilivyokwisha kukomaa kutoka nje au kwenye akademi chache zinazopatikana.nchini.

Vilabu vikubwa nchini Tanzania Simba na Yanga vinatakiwa kuiga mfano wa klabu ya FC Barcelona ya Hispania kwa kuwa na academy imara iliyo ibua vipaji vikubwa na vinavyoimbwa Kila siku Duniani , kitu ambacho huwa kinawapunguzia gharama za kusajili kwa kusaini wachezaji ndani ya academy Yao ya lamasia mfano wa mazao Yao ni Lionel Messi na Lamine Yamal, hawa ni kwa uchache.

Hivyo ni jukumu la TFF na vilabu nchini kukaa na kutathimini ni hatua zipi watakazo zichukua ili kuweka njia Bora kwaajili ya kuwapika vijana ili kutengeneza hadhina ya Taifa kwenye michezo nchini.


0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.

.


0/Post a Comment/Comments