Timothy lugembe;
Mwanakwetusports.
Klabu ya Simba SC imekamilisha usajili wa mshambuliaji kutokea Singida black stars Jonathan Sowah , hatua ambayo inalenga kuimarisha kikosi chao kuelekea msimu ujao wa mashindano.
Sowah ni mshambuliaji hatari na mwenye uchu wa magoli ambapo msimu uliopita akiwa na klabu yake ya Singida alipachika jumla ya mabao 13, nyuma ya Clement mzize wa Yanga aliiekuwa na magoli 14 na Ahoua wa Simba goli 16, na mabao hayo yote aliyafunga kwa kucheza nusu ya msimu ukulinganisha na wachezaji wengine walioanza tangu mwanzoni mwa msimu hali inayo onyesha uhatari wake.
Klabu ya Simba ilimfuata mshambuliaji huyo kwa mradi maalumu uliopo klabu hapo ikiwa ni kuhakikisha timu inapata maendeleo , jambo ambalo lilimshawishi mshambuliaji huyo na kuchagua kujiunga kwenye jeshi la nyekundu na nyeupe.
Usajili huu umemuweka matatani mshambuliaji wa Simba Ateba Mbida aambapo inatajwa kuwa klabu kutokea nchini Morocco Maghereb of fez, imeweka ofa kubwa kwaajili ya kumnasa mshambuliaji huyo kinacho subiriawa ni klabu kuridhia ofa au kukataa.
0767915473,
Lugmbetimothy01@gmail.com.
Post a Comment