SIRI YA KIBU NA MAJARIBIO MAREKANI

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mchezaji nyota wa Simba SC, Kibu Dennis, yupo mbioni kumaliza majaribio yake ya wiki tatu ndani ya klabu ya Nashville SC inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani (MLS).

Awali, Nashville SC walimpa Kibu kipindi cha wiki mbili kwa ajili ya majaribio, lakini klabu hiyo iliamua kumuaongezea wiki Moja zaidi kwaajili ya kuzidi kuangalia kiwango Cha mchezaji huyo,

Chanzo cha karibu na mchezaji huyo kimesema kuwa Kibu anapigania ndoto yake ya kucheza soka nchini Marekani ili awe karibu na familia yake inayoishi huko ambapo yeye muda mwingi anakuwa Tanzania kuitumikia klabu yake ya Simba Sc, licha ya kuwepo kwa ofa nyingine nono kutoka klabu ya MC Alger ya Algeria lakini kibu ameamua kupambana kubaki Marekani yote hiyo kwaajili ya kuwa karibu na familia.

Mapema siku chache kibu hakuweza kujiunga na timu ya Taifa ya Tanzania kuelekea mashindano ya CHAN yanayohusisha wachezaji wanaocheza ligi ya ndani , kwasababu ya kutaka kutimiza ndoto yake ya kucheza Marekani, mpaka hatua ya kushindwa kujiunga na timu ya Taifa inaonyesha dhamira ya dhati ya mchezaji huyo kutaka kuwa karibu na familia yake.

Nashville SC ni mojawapo ya timu imara katika MLS, kwa sasa ikishikilia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo ya Marekani, Mafanikio ya Kibu kwenye majaribio hayo yanaweza kufungua milango mipya ya mafanikio, kwani kama atafanya vizuri, klabu hiyo itatuma ofa rasmi kwa Simba SC ili kumsajili kiungo huyo mahiri.

Iwapo Kibu atafanikiwa kujiunga na Nashville SC, basi atakuwa mmoja wa wachezaji wachache wa Tanzania waliopata nafasi ya kucheza katika ligi kubwa kama MLS, hatua itakayoongeza heshima kwa taifa na Simba SC kwa ujumla.

0767915473.

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments