Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi zawadi ya shilingi Billioni moja endapo kama timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ikitwaa ubingwa wa CHAN mashindano yanayo husisha wachezaji wanao cheza ligi za ndani yatakayo kwenye nchi tatu Tanzania, Kenya , na Uganda.
Kauli hiyo iliwasilishwa na waziri wa habari Sanaa na michezo Prof. Paramagamba Kabudi wakati akiongea na waandashi wa habari kuhusu maswala ya kimichezo katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es laam .
Hii inaongeza chachu ya ushindani kuelekea kuanza kwa mashindano hayo ambapo Tanzania itahusika kwenye mchezo wa ufunguzi dhidi ya Burkinafaso siku ya july 2 mwaka huu, safari ya kuilekea billioni moja itaanza kupambaniwa rasmi kwenye mchezo huo wa ufunguzi huku ushindi ndio itakuwa ni ishara nzuri kuelekea kuchukua kitita hicho.
Hii sio mara ya kwanza kwa Rais. Samia kutoa ahadi nono kwenye mpira wa miguu ikumbukwe yeye ndio chachu ya vilabu vikubwa nchini , Simba na Yanga kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa kupitia hamasa ya (goli la mama), pia hata timu ya Taifa kufuzu mashindano ya AFCON mara kadhaa mchango wa Raisi umehusika kwa asilimia kubwa.
Kazi iliyobaki ni kwa wadau na mashibiki kuhakikisha wanatoa hamasa kwa timu ya Taifa inakuwa kubwa kuelekea safari hiyo ya mashindano, washabiki wanatakiwa kujitokeza kwa wingi viwanjani kuhakikisha kikombe hiki kinabaki nchini kwa heshima ya soka la Taifa letu.
0767915473.
Lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment