RS BERKANE WABISHA HODI KWA MPANZU

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya RS Berkane kutoka Morocco ipo mbioni kupeleka ofa ya usajili wa kiungo wa Simba SC, Elie Mpanzu, baada ya kuanza mazungumzo ya awali na wawakilishi wa mchezaji huyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa watu wa karibu na dili hilo, Berkane bado hawajaiwasilisha ofa rasmi kwa Simba SC, wakisubiri kwanza kufikia makubaliano binafsi na Mpanzu kuhusu masuala ya mshahara pamoja na bonasi atakazopokea akijiunga na timu hiyo.

Ripoti zinaeleza kuwa RS Berkane wako tayari kulipa kiasi cha takribani Shilingi milioni 450 za Kitanzania, ambacho ni kipengele cha kuvunja mkataba (“release clause”) kilichowekwa na Simba kwenye mkataba wa Mpanzu, endapo kuna timu itataka kumsajili kabla ya muda wake kumalizika.

Hali hiyo inaashiria uwezekano mkubwa wa kiungo huyo kuagana na Wekundu wa Msimbazi, endapo mazungumzo binafsi yatafanikiwa na ofa rasmi itawasilishwa mezani.

Hii ni kengele ya tahadhari kwa Simba kuelekea msimu mpya , inabidi wafanye usajili wa wachezaji wenye viwango zaidi ili kuzuia kuyumba kwa timu yao au laa wanahitajika kutoa ofa nono ili kuwa bakisha wachezaji wao muhimu ambao wanawindwa na vilabu vikubwa kama Elie Mpanzu.



0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments