RASMI MUSONDA AWAAGA WANANCHI


 Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mshambuliaji  wa Yanga SC, Kennedy Musonda, ameaga rasmi klabu hiyo kwa ujumbe wa kugusa hisia uliowagusa mashabiki wa timu hiyo na wadau wa soka kwa ujumla.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Musonda alionesha shukrani za dhati kwa mashabiki, viongozi wa klabu, familia yake, na wote waliomuunga mkono wakati wa kipindi chake ndani ya miamba hiyo ya soka Tanzania, Katika ujumbe wake wa hisia, Musonda aliandika:

“Wananchi, niseme nini? Mmekuwa bora sana kwangu, kwa familia yangu na kwa ndoto yangu. Asanteni kwa kucheka nami, kuota nami, kushinda nami, na pia kwa kulia nami.”

Aliendelea kuonesha upendo na uaminifu wake kwa klabu hiyo, akihitimisha kwa kusema:

“Mtu mmoja alisema kila hadithi nzuri lazima iishe, Nitawashukuru daima, Sasa ni wakati wa kuanza ukurasa mwingine.”

Mpaka anaondoka klabuni hapo ameifungia timu yake magoli 34 na pasi za kusaidia magoli (assist) 13 huku mafanikio mengine aliyoyapata ni pamoja na Kutwaa vikombe vya ligi kuu na kufika fainali ya kombe la shirikisho.

mpaka sasa Musonda ndiye mchezaji aliethibitisha kuwa msimu ujao hatakuwa na wananchi hata kabla ya timu hiyo kuanza kutoa Asante kwa wachezaji wao ambao msimu ujao hawatakuwa pamoja nao. je ,ni nani na nani wanafuata kuagwa klabuni hapo?



0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.

0/Post a Comment/Comments