Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Azam FC rasmi imethibitisha kumteua Florent Ibenge kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo, ikilenga kuongeza ushindani kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa.
Ibenge, ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR Congo), anachukua mikoba hiyo huku akibeba matumaini makubwa kutoka kwa mashabiki na uongozi wa Azam FC kutokana na uzoefu wake mkubwa katika soka la Afrika, Taarifa za kuhusishwa kwa Ibenge na Azam FC zimekuwa zikisambaa kwa wiki kadhaa, lakini sasa klabu hiyo imeweka mambo wazi kwa kuthibitisha kuwa makubaliano rasmi yamekamilika.
Ibenge anatarajiwa kuanza kazi mara moja kwa kuongoza mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya, huku akikabidhiwa jukumu la kuhakikisha Azam FC inarejea kwenye ubora wake na kupigania taji la Ligi Kuu dhidi ya wapinzani wakubwa kama Yanga SC na Simba SC.
Azam FC imekuwa ikifanya maboresho makubwa ndani ya kikosi chake, na ujio wa Ibenge ni sehemu ya mkakati mpana wa kuimarisha timu hiyo kuelekea msimu wa 2025/2026. Mashabiki wa soka nchini sasa wana macho kwa Azam, wakisubiri kuona namna Ibenge atakavyobadilisha mwenendo wa timu hiyo.
0767915473.
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment