RASMI FEI AKUBALI KUJIUNGA NA MYAMA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

 Kiungo mshambuliaji mwenye kipaji cha hali ya juu, Feisal Salum maarufu kama Fei Toto, amekubali kujiunga na klabu ya Simba SC, ambapo amepanga kusaini mkataba wa miaka miwili mara tu hatua za mwisho zitakapokamilika.

Taarifa kutoka kwa vyanzo vya karibu na mchezaji huyo zinasema kuwa tayari amewasiliana na uongozi wa Azam FC kuufahamisha kuwa hataongeza mkataba mpya, huku akisisitiza kuwa huo ndiyo uamuzi wake wa mwisho.

Inadaiwa kuwa namba yake maarufu ya jezi itakuwa miongoni mwa vitu atakavyovivaa pindi atakapothibitishwa rasmi kuwa mchezaji wa Msimbazi, jambo linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Simba SC.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Feisal ameshafikia makubaliano binafsi na Simba SC, ambapo amevutiwa sana na mpango wa kocha wa timu hiyo, Fadlu Davids, na ndoto yake kuu ikiwa ni kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na Wekundu wa Msimbazi licha ya kocha wa Azam fc Kumzuia Fei kuondoka lakini Fei hajawa tayali kusalia klabuni hapo na sasa anataka kuondoka.

Hata hivyo, hatua inayofuata ni kwa Simba SC kufikia mwafaka rasmi na Azam FC kuhusu uhamisho wake, au Feisal mwenyewe kuanza mazungumzo ya kuondoka kwa maridhiano ya hiaribkutoka Azam fc.

Ikiwa dili hili litakamilika, basi Simba itakuwa imepiga hatua kubwa katika dirisha hili la usajili kwa kumpata kiungo ambaye kwa muda mrefu amekuwa akiwindwa na klabu kadhaa kutokana na uwezo wake mkubwa uwanjani, hatua hii inalenga kujenga kikosi Cha wekundu wa msimbazi kuelekea mashindano ya kimataifa.



0767915473.

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments