Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Katika mchezo wa marudiano wa mchujo wa kuwania kubaki kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, timu ya Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika uwanja wa Sokoine dhidi ya Fountain Gate FC, hivyo kufuzu kwa jumla ya mabao 4-2 (agg 4-2) baada ya mchezo wa kwanza kumalizika kwa sare ya 1-1.
Mechi hiyo ya kusisimua iliwavutia mashabiki wengi waliokuwa na hamu ya kujua hatma ya vikosi hivyo viwili. Prisons walitumia vyema faida ya kuwa nyumbani kwa kutumia mbinu zilizozalisha mabao matatu yaliyowapa uhai mpya ,Kwa matokeo hayo, Tanzania Prisons wamethibitisha rasmi kuwa wataendelea kushiriki michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/2026.
Hata hivyo, hali ni tofauti kwa Fountain Gate ambao sasa wanatakiwa kuchuana na Stand United katika hatua nyingine ya mchujo (play-off) ili kuwania nafasi ya mwisho ya kujiunga na Ligi Kuu.
Mchezo huo kati ya Fountain Gate na Stand United unatarajiwa kuwa wa aina yake, kwa kuwa kila timu itakuwa na kiu ya kupambana kwa nguvu zote kuhakikisha inatinga ligi kuu. Ushindi kwa upande wowote utakuwa na maana kubwa kwa klabu na mashabiki wao.
katika mchezo unaofata ambapo Fountain gate wataenda kutetemeka nafasi Yao KUCHEZA ligikuu watachuana na Stand united huku nafasi kubwa wakipewa fountain gate kutokana na kucheza michuano ya ligi kuu na uzoefu.
0767915473.
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment