PREMIER LEAGUE KUBORESHWA: MABADILIKO MAKUBWA KWA MSIMU MPYA

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Katika hatua ya kuvutia mashabiki na kuongeza mvuto wa mechi, uongozi wa Ligi Kuu ya England (Premier League) umetangaza rasmi mabadiliko mapya yatakayoanza kutekelezwa msimu ujao.

Mabadiliko hayo yanalenga kuongeza maudhui ya moja kwa moja kwa mashabiki na kuwapa hisia za karibu zaidi na matukio yanayojiri ndani na nje ya uwanja. Mabadiliko hayo rasmi ni kama ifuatavyo:

 Mahojiano ya wakati wa mapumziko (halftime),  Mashabiki watapata fursa ya kusikia maoni ya wachezaji na makocha wakati wa mapumziko ya mechi, Hatua hii inalenga kuwapa watazamaji mtazamo wa moja kwa moja juu ya hali ya mchezo kutoka kwa wahusika wakuu.

 Mahojiano na wachezaji wanaotolewa uwanjani,  Mara baada ya mchezaji kutolewa uwanjani, atahojiwa moja kwa moja kuhusu mchezo na hali yake binafsi. Hii itasaidia kufahamu maoni ya mchezaji akiwa bado na hisia hai za mchezo.

 Matangazo ya moja kwa moja kutoka vyumbani kwa wachezaji (dressing room broadcasts), Kwa mara ya kwanza, mashabiki watapata mwanga wa kile kinachoendelea katika vyumba vya kubadilishia nguo wakati wa mapumziko au baada ya mechi, hatua inayotarajiwa kuleta msisimko mkubwa.

Hii ni sehemu ya mkakati wa Premier League kuboresha uzoefu wa mashabiki na kuleta mapinduzi katika utangazaji wa soka kwa kiwango cha juu.

Hatua hizi mpya zimepokelewa kwa hisia tofauti, baadhi wakiziona kama njia ya kuimarisha burudani na uwazi, huku wengine wakihofia athari kwa wachezaji na makocha.

Mashabiki duniani kote wanasubiri kwa hamu kuona jinsi mabadiliko haya yatakavyotekelezwa uwanjani na kamera zitakavyofichua upande mwingine wa mchezo ambao haukuwahi kuonekana

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.

0/Post a Comment/Comments