Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Taifa limeguswa kwa huzuni na msiba wa Mzee Samatta, baba mzazi wa mshambuliaji nyota wa zamani wa Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta, aliyefariki dunia mapema asubuhi ya leo Jumapili Julai 6 , akiwa nyumbani kwake, Mbagala jijini Dar es Salaam,Taarifa za kifo chake zimedhibitishwa na mtoto wake mkubwa, Mohamed Samatta.
Katika enzi za uhai wake, Mzee Samatta alikuwa mchezaji wa soka mwenye kipaji kikubwa, akiitumikia timu ya taifa na vilabu kadhaa vya ndani ya nchi, Alitumia jezi namba 10, nafasi ya ushambuliaji aliyokuwa akiimiliki kwa ustadi mkubwa, Rekodi zinaonyesha kuwa alikuwa mshambuliaji hatari, aliyewahi kutikisa vilabu pinzani kwa mabao yake ya kuvutia.
Mbali na uchezaji wake uwanjani, Mzee Samatta alikuwa mtu maarufu katika jamii ya Mbagala. Alijijengea heshima kutokana na maadili na malezi bora aliyoyatoa kwa familia yake, Wengi wanamkumbuka kwa busara zake na msimamo wa kulea watoto wake katika msingi wa nidhamu na bidii, jambo ambalo limezaa matunda makubwa kupitia mafanikio ya Mbwana Samatta nembo ya soka la Tanzania kimataifa.
Wanasoka, viongozi wa michezo, mashabiki, na wanajamii wameendelea kumiminika nyumbani kwa familia hiyo kutoa pole, Klabu mbalimbali nchini, pamoja na mashabiki wa TP Mazembe, na Simba SC, wametuma salamu za rambirambi mitandaoni, wakimtaja marehemu kama shujaa wa soka ambaye mchango wake utaendelea kukumbukwa vizazi na vizazi.
Mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho jioni kwa mujibu wa taratibu za familia, na viongozi wa serikali pamoja na wanamichezo wanatarajiwa kuhudhuria, pumzika kwa amani mzee Ally Pazia Samatta.
0767915473.
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment