PEP GUARDIOLA KUPUMZIKA KULINDA AFYA YAKE


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kocha mahiri wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola, ametangaza kuwa atachukua mapumziko ya muda mfupi mara baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Manchester city ya Uingereza.

 Guardiola ambaye ni raia wa Hispania, amesema kuwa anahitaji muda wa kupumzika ili kuutuliza mwili wake na pia kuangalia afya yake pamoja na maisha yake binafsi baada ya muda mrefu wa kuwa katika majukumu ya ukocha.

Guardiola, ambaye ameiongoza Manchester City kwa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kutwaa mataji ya Ligi Kuu ya England na Ligi ya Mabingwa Ulaya, amekuwa moja ya makocha waliovuna mafanikio makubwa barani Ulaya katika kipindi cha hivi karibuni.

Katika taarifa yake, Guardiola alisisitiza kuwa licha ya mapenzi yake kwa mchezo wa soka, ni muhimu kujitunza kiafya na kuwa na muda wa kujipumzisha kabla ya kufikiria majukumu mengine ya kazi.

Mashabiki wa Manchester City na wadau wa soka duniani kote wameshangazwa na uamuzi huo lakini pia wamempongeza kwa maamuzi ya busara yanayozingatia afya na ustawi binafsi.



0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments