PALACE YASHUSHWA CONFERENCE, NOTTINGHAM KUCHEZA EUROPA

 


SABABU NI UKIUKWAJI WA KANUNI ZA UMILIKI WA VILABU.

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Ndoto ya Crystal Palace kucheza Europa League msimu ujao imeshindikana baada ya UEFA kuitupilia mbali nafasi yao kutokana na ukiukwaji wa kanuni za umiliki wa vilabu vinavyoshiriki mashindano ya Ulaya.

 Hii ni baada ya kugundulika kuwa mmiliki mwenza wa Palace, John Textor, pia anamiliki hisa katika vilabu vingine vinavyoshiriki mashindano hayo, ambayo ni Klabu ya Olympic Lyon ya ufaransa , Lyon watashiriki Europa kwasababu wote pamoja na palace walifuzu kushiriki mashindano hayo kutokana na kanuni palace wameshushwa Hadi conference league na Lyon kushiriki Europa.

Hatua hii imetokea wakati klabu ya Lyon, inayomilikiwa pia na Textor, ilipokumbwa na matatizo ya kifedha na kutangazwa kushushwa daraja na chombo cha usimamizi wa fedha cha soka la Ufaransa DNCG mwezi Novemba, kabla ya kushinda rufaa yao na kubaki Ligue 1, Hali hiyo iliweka mazingira tata kwenye nafasi ya Palace kwenye ushiriki wake wa Europa league.

Kwa sasa, Palace wanaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo ,lakini kama uamuzi wa UEFA utadumu, Nottingham Forest wamechukua nafasi ya palace katika mashindano ya Europa League, Forest walimaliza nafasi ya saba msimu uliopita na awali walistahili kucheza UEFA Conference League.

Hii ni pigo kwa mashabiki wa Palace waliokuwa wakitamani kuona klabu yao ikirejea kwenye ramani ya soka la Ulaya, lakini pia ni fundisho kwa wawekezaji kuzingatia na kufuata kanuni za Umiliki sawa sawa na maelekezo ya UEFA.



0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments