NIGERIA MABINGWA WAFCON, WAIKALISHA MORROKO NYUMBANI KWAKE

 


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Timu ya taifa ya wanawake ya Nigeria, Super Falcons, imeandika historia nyingine kwa kutwaa taji lao la 10 la TotalEnergies Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji Morocco kwenye Uwanja wa Stade Olympique jijini Rabat, usiku wa Jumamosi Julai 26.

Nigeria ilijikuta nyuma kwa mabao 2-0 hadi mapumziko, mbele ya mashabiki wa Morocco waliokuwa wakisubiri kuona timu yao ikiweka historia kwa kutwaa ubingwa ubingwa kwenye ardhi ya nyumbani , Lakini Super Falcons walionyesha dhamira, uzoefu na moyo wa ushindani kwa kurudi kwa kishindo na kugeuza matokeo hayo kuwa ushindi.

Morocco walitangulia mapema dakika ya 12 kupitia nahodha wao Ghizlane Chebbak aliyefunga kwa shuti kali nje ya boksi lililompita kipa wa Nigeria, Chiamaka Nnadozie, Morocco waliongeza bao la pili dakika ya 24 kupitia Sanaâ Mssoudy baada ya pasi nzuri kutoka kwa Ibtissam Jraidi.

Magoli ya Nigeria yalifungwa na Esther Okoronkwo (kwa mkwaju wa penalti), Folashade Ijamilusi, na bao la ushindi dakika ya 88 lililofungwa na Joe Echegini, wakiiweka Nigeria kileleni kwa mara ya 10 kati ya mashindano 13 yaliyowahi kuchezwa.

Licha ya mashambulizi ya dakika za mwisho kutoka kwa Morocco, lakini Nigeria walihimili na kuhakikisha wanalinda ushindi wao , Kocha wa Morocco, Jorge Vilda, aliwapongeza wachezaji wake kwa kutinga fainali lakini akaeleza masikitiko ya kushindwa kufanikisha ndoto ya kutwaa taji hilo mbele ya mashabiki wao.

Kwa ushindi huo, Nigeria inaendelea kuonyesha ubabe wake katika soka la wanawake barani Afrika, na kuthibitisha kuwa wao bado ni timu ya kuogopwa licha ya ushindani unaozidi kuongezeka kutoka kwa mataifa mengine.

Nigeria ndio iliyo twaa kikombe hiki mara nyingi zaidi ikiwa imetwaa mara kumi kati na mara kumitatu ambayo ndio idadi kamili ya mashindano hayo.


0767915473.

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments