NAHODHA MELI YA YANGA APATIKANA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Yanga Africans imethibitisha usajili wa kocha kijana Zaidi Romain Folz mwenye umri wa miaka (35), amabaye ni mzaliwa wa Bordeaux ufaransa , anaamini katika mfumo wa ( 4-3-3), na katika leseni za ukocha anamiliki UEFA Pro licence.

Mbali ya kuwa kocha kabala ya kutua jangwani alikuwa mkurugenzi wa michezo wa Olympique Akbou ya nchini Algeria kitu kinacho onyesha mbali na kuwa mkufunzi pia anao ustadi wa kuwa kiongozi kwenye masuala ya mpira wa miguu.

UZOEFU WA FOLZ NA SOKA LA AFRICA

1: 2018 – Alikuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Uganda

2: 2019 – Alikuwa kocha msaidizi wa Pyramid kutokea Egypt

3: 2021 – Alikuwa kocha mkuu wa timu ya Township Rollers ya Botswana

4: 2022- Alikuwa kocha mkuu wa Amazulu ya Afrika kusini

5: 2023 – Alikuwa kocha mkuu wa Horoya ya nchini Guinea

6: 2024 – Alikuwa kocha msaidizi wa Mamelod sundown ya Afrika kusini

7: 2025 – Alikuwa mkurugenzi wa michezo wa Olympique Akbou ya Algeria.

Na kwa sasa kocha huyo kajiunga na wananchi kuelekea msimu mpya wa mashindano mashabiki na wadau wa michezo nchini wanaamini kuwa uzoefu wa kocha huyo kwenye soka la Afrika sambamba na umri wake mdogo atawafikisha mbali hasa hasa kwenye mashindano ya Afrika.

0767915473,

Lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments