Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Simba Sports Club imepoteza mlinzi wa pembeni imara katika dirisha la usajili baada ya beki wake wa kimataifa kutoka Burkina Faso, Valentin Nouma, kuondoka rasmi klabuni hapo.
Nouma, ambaye alijiunga na wekundu wa Msimbazi kwa matarajio makubwa ya kuimarisha safu ya ulinzi, kwa kusaidiana na Zimbwe ,sasa ameagana na mashabiki wa Simba SC baada ya kutamatisha rasmi mkataba wake, Taarifa kutoka ndani ya klabu zinaeleza kuwa beki huyo ataendelea na maisha ya soka msimu ujao katika klabu mpya nje ya Tanzania.
Kwa kipindi chake akiwa Simba SC, Nouma alijitahidi kuonesha uwezo mkubwa uwanjani, akihusika katika michezo mbalimbali ya ndani na kimataifa, Hata hivyo, uongozi wa klabu haujatoa sababu rasmi za kuondoka kwake, lakini vyanzo vinaeleza kuwa ni makubaliano ya pande zote mbili.
Kuondoka kwa Nouma kunamaanisha Simba italazimika kuimarisha eneo la ulinzi kuelekea msimu mpya, hasa ikizingatiwa kuwa klabu hiyo inatarajiwa kushiriki michuano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
Hata hivyo imekuwa ngumu sana kwa misimu kadhaa wachezaji wanaokuja Simba kudumu kwenye nafasi za ulinzi wa pembeni ambapo wachezaji wengi wa kimataifa wamekuja lakini hawajafanikiwa kuchukua namba mbele ya Zimbwe Jr na Shomari kapombe hii inazidi kuonyesha jinsi gani wachezaji Hawa ni roho ya Klabu ya Simba sc.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment