Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Bayern Munich imethibitisha kuwa kiungo , Jamal Musiala, ataukosa uwanja kwa kipindi Cha miezi mitano baada ya kuvunjika miguu huku kifundo cha mguu kiligeuka katika mchezo wa Klabu Bingwa ya Dunia dhidi ya Paris Saint-Germain uliochezwa Julai 5..
Musiala mwenye umri wa miaka 22 aliumia vibaya katika kipindi cha kwanza wakati akijaribu kufukuzia mpira karibu na mstari wa goli, kabla ya kugongana na kipa wa PSG, Gianluigi Donnarumma, Punde tu baada ya kuguswa, Musiala alisikika akipiga yowe kali kwa maumivu, akishika kifundo cha mguu wake wa kushoto huku akijifunika uso wake kwa jezi alipokuwa akitolewa nje kwa machela.
Taarifa rasmi kutoka klabu ya Bayern Munich imesema kuwa mchezaji huyo alikimbizwa hospitalini kwa uchunguzi wa kina kabla ya kusafirishwa kurejea mjini Munich kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji maalum.
Jeraha hilo linakuja wakati ambao Musiala alikuwa akirejea katika ubora wake baada ya kukosa mechi kadhaa msimu huu kutokana na majeraha ya misuli. Sasa Bayern Munich itakabiliwa na kibarua kigumu kuhimili pengo lake katika mbio za kutafuta mafanikio ndani na nje ya Ujerumani.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment