Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa stars) imeonekana kuimarika kiuchezaji kuelekea michuanao ya CHAN ambayo inatarajiwa kuanza Agost ,2 katiak nchi tatu za Africa Mashariki ambazo ni Kenya , Uganda , na Tanzania , katika mchezo wa ufunguzi Stars ita menyana na Burkinafaso kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es laam.
Uimara wa Staars umeonekana kupitia mashindano ya CECAFA yaliyo husisha nchi tatu amabazo ni Tanzania, Uganda na Senegali katika maaandalizi kuelekea CHAN yaliyo fanyika Karatu jijini Arusha, katika mashindano hayo Stars imefanya vizuri kwa kupata ushindi katika michezo yote miwili waliyoshiriki.
Katika mchezo wa kwanza Stars walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Uganda bao liliwekwa kimiani na Iddy Nado, katika mchezo wa pili uliofanyika jana waliichapa Senegal bao 2-1, katika mchezo huo Senegal walianza kuliona lango mapema dakika ya 8’ kupia kwa Mbodji, na baadae kipindi cha pili Stars walisawazisha kupitia kwa Suileiman Sopu kwa mkwaju wa penati dakika ya 53’ na bao la ushindi likifungwa na Ibrahim Hamad Bacca dakikka ya 56’ .
Kwa upande wa kocha wa Stars Hemed Suleimain amesema kuwa wamefanikiwa kwa asilimia 80 katika michezo hiyo miwili huku akikili kuwa kuna mambo ambayo bado hayajakaa sawa na wanarudi Dar es laam kwaajili yakuendelea kujipanga kwa siku nne zilizobaki ili kuweka mambo sawa kabala mchezo wao ufunguzi.
‘’kwanza namshukuru Mungu tumemaliza mechi salama na ninafikili tumefanikiwa kwa asilimia 80 kwa hizi mechi mbili ila bado kuna mambo hayaenda vizuri kwenye baadhi ya maeneo tunahitaji kuyafanyia kazi kabla ya kuanza mechi tarehe pili, tunaendea kujipanga kuhakikisha tunashinda haya mashindano nafkiri ndoto ya kila mTanzania iko hivyo kwahivyo tunarudi nyumbani kesho tunasiku nne za kurekebisha mapungufu yaliyo onekana katika michezo hii miwili na ninaamini kwa kikosi tulichonacho wachezaji wana adopt vizuri na siku ya mechi tutakuwa vizuri na tutapata matokeo’’ alisema kocha Hemed.
Kuelekea mashindano hayo mashabiki na wadau wa soka nchini wanaa amini kuwa timu yao itafanya vizuri kwani kwa upande wa ligi za ndani ligi ya Tanzania ipo juu ukilinganisha na baadhi ya timu kwenye mashindano hayo na ndiyo ligi inayo ongoza kwa kukuza vipaji sio tu vya wachezaji wa ndani pia hata wanaotoka nje ya nchi wanatumia ligi hiyo kama daraja kuvusha kuwapeleka mbali Zaidi.
Kinacho subiriwa ni kuanza kwa mashindano na kuipima ligi yetu kuona je, inafaa kuwa nafasi iliyopo majibu yatapatikana pale michuano itakapo anza kutimua vumbi.
0767915473,
Lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment