Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Michezo ni shughuli za mwili au akili zinazofanywa kwa lengo la kushindana au kwa kujifurahisha, ambazo huchangia katika maendeleo ya kimwili, kiakili na kijamii, Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, michezo ni sehemu ya mazoezi ya mwili yanayosaidia mwili kufanya kazi vizuri, kuhimili uchovu na kuongeza ufanisi wa viungo mwilini.
Katika ulimwengu wa sasa unaokabiliwa na changamoto nyingi za kiafya kutokana na mtindo wa maisha usio na mazoezi, michezo inachukuliwa kuwa tiba na njia bora ya kuimarisha afya kwa njia ya asili na isiyo na madhara.
Michezo ina uhusiano wa moja kwa moja na afya ya binadamu , Kwa kuwa mwanamichezo, unafanya mwili kupata mazoezi ya kutosha ambayo huongeza mzunguko mzuri wa damu, hupunguza mafuta mwilini, na huimarisha moyo pamoja na mapafu, pia michezo huongeza uwezo wa mwili kujikinga dhidi ya magonjwa kwa kuboresha mfumo wa kinga mwilini.
FAIDA ZA MICHEZO KWA AFYA YA BINADAMU
1. Huimarisha afya ya moyo , Michezo husaidia kudhibiti shinikizo la damu na kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo.
2. Hupunguza msongo wa mawazo , Michezo huongeza kemikali za furaha kama endorphins, ambazo hupunguza msongo wa mawazo.
3. Huimarisha mifupa na misuli , Mazoezi ya mara kwa mara hupunguza uwezekano wa kupata magonjwa kama osteoarthritis.
4. Hudhibiti uzito , Michezo huchoma kalori nyingi, hivyo kusaidia kudhibiti uzito wa mwili.
5. Huongeza usingizi mzuri , Wanaoshiriki michezo hupata usingizi wa kutosha na wenye utulivu.
6. Huongeza uwezo wa akili , Michezo ya kiakili kama vile chess huongeza umakini na kumbukumbu.
7. Huongeza kujiamini , Mafanikio katika michezo hujenga hali ya kujiamini na kuthamini uwezo binafsi.
Kwaajili ya ustawi wa afya zetu tusiache kufanya mazoezi walau mara tatu kwa siku hiyo itatusaidia kujiweka sawa kimwili na kiakili michezo ni afya tuthamini kufanya mazoezi.
0767915473.
lugembetimothy01@gmail.com..
Post a Comment