MIAKA 11 IMETOSHA, MACHO NA MASIKIO JANGWANI

 


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Nahodha wa zamani wa Simba SC, Mohamed Hussein maarufu kama “Zimbwe Jr”, ametangaza kuaga rasmi klabu hiyo baada ya takribani miaka 11 ya kuitumikia kwa uaminifu, kujituma na kupigania mafanikio ya timu hiyo kubwa ya soka nchini Tanzania.

Kupitia taarifa rasmi aliyoitoa, Mohamed Hussein amesema uamuzi wake umetokana na kutaka kuendelea na maendeleo yake binafsi na kulinda maslahi pamoja na taaluma yake ya kitaaluma katika soka, Ameeleza kuwa kipindi chote cha miaka 11 ndani ya kikosi cha Simba kimekuwa na furaha, huzuni, nderemo, vifijo na changamoto mbalimbali, lakini aliendelea kuwa imara kutokana na mapenzi yake kwa nembo ya klabu hiyo.

“Kwa uaminifu mkubwa, weledi na kiwango cha juu, kuvujisha jasho kuipigania nembo ya klabu ndio ulikuwa msingi na malengo yangu,” alisema Hussein katika ujumbe wake wa kuaga.

Katika andiko lake, Zimbwe hakusita kuwashukuru viongozi wa klabu hiyo, benchi la ufundi, wafanyakazi wote wa Simba SC pamoja na mashabiki kwa ushirikiano mkubwa waliompa tangu aanze kuitumikia timu hiyo, Pia aliwashukuru viongozi wa menejimenti ya klabu ikiongozwa na Carlos Carlos kwa namna walivyoshirikiana naye kwa kipindi chote akiwa mchezaji ndani ya klabu hiyo.

Mohamed Hussein alikuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya Simba SC kwa zaidi ya muongo mmoja, akisaidia timu kutwaa mataji ya Ligi Kuu Tanzania Bara na kushiriki michuano ya kimataifa kama Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa taarifa zilizopo Zimbwe alikuwa tayali kuongeza mkataba klabuni hapo lakini uongozi ulichelewesha mipango huo nakumfanya sasa Zimbwe kutafuta changamoto mpya kinachosubiriwa ni je ,atajiunga na wananchi .

Kwa kipindi Cha miaka ya hivi karibuni klabu ya Yanga imekuwa ikichukuwa wachezaji muhimu kutoka kwenye kikosi Cha Simba bila pingamizi kwa kuanza walimchukua clatous Chama, na Jonas Mkude na hivi sasa Hatua itayo waumiza Wana Simba ni kusikia Zimbwe anasaini klabuni hapo.

Je, Nini kinacho Wanafanya Simba kushindwa kubakiza wachezaji imara kwenye kikosi chao na badala yake wanaondoka kama wachezaji huru shida ipo wapi?



0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments