MFUPA ULIOWASHINDA VIGOGO ULAYA UMELIKA DARAJANI

CHELSEA WABEBA NDOO, PSG WABAKI MIDOMO WAZI

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Timu ya Chelsea kutokea nchini Uingereza imaeushangaza ulimwengu wa soka kwa kuwatandika PSG ya nchini ufaransa kwa Jumla ya bao 3-0 na Kutwaa taji la vilabu Duniani kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la MetLife stadium huku mgeni rasmi akiwa Rais wa Marekani Donald Trump.

Katika mchezo huo Chelsea waliutawala mchezo kuanzia dakika ya kwanza na kuwafanya kupata mabao matatu na ya pekee kipindi Cha kwanza , mabao hayo yaliwekwa kimiani na Palmer 22' na 30' huku msumari wa mwisho ukipigiliwa na Joao Pedro 43' Hadi dakika tisini zinatamatika Chelsea 3-0 Paris saint Germain.

Toka mashindano yameanza timu iliyokuwa ikipewa nafasi ya Kutwaa taji hili ni PSG na keuleka fainali hii PSG walitarajiwa Kutwaa kikombe hiki baada ya kuuwadhibu vigogo barani ulaya ikiwemo Real Madrid 4-0, wakawaadhibu Bayern Munich 2-0, na katika mashindano ya UEFA champions league fainali waliwaadhibu inter Milan 5-0, lakini isivyo tarajiwa klabu ya Chelsea imaeushangaza ulimwengu kwa kuvunja utawala wa PSG barani ulaya na Kutwaa ubingwa huo.

Hii ni mara ya pili kwa Chelsea Kutwaa taji hili baada ya mwaka 2022 chini ya kocha Thomas Tuchel kufanya hivyo, na hili linakuwa taji lao la pili mwaka huu baada ya kuchukua Conference league mbele ya Bets na umekuwa msimu wenye neema na mafanikio kwao chini ya kocha Enzo Maresca.

Licha ya kuupoteza mchezo wa fainali kwa PSG lakini umekuwa ni mwaka wenye mafanikio makubwa toka kuanzishwa kwake kwa Kutwaa vikombe vya ligi nchini ufaransa pia kuchukua UEFA kwa mara ya kwanza .

Mchezo wa soka unamatokeo matatu na siku zote mpira unadunda na unamaajabu yake na huu umekuwa muendelezo tu Kila fainali anayoingia Chelsea kama timu ya pili ( underdog) wamechukua .



0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments