MATAIFA MATATU KUJINOA KUELEKEA CHAN

 

Timothy Lugembe ,

Mwanakwetusports.

Katika kuhakikisha timu za Taifa zinajiandaa na kuwa tayari kwa mashindano ya CHAN, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na CECAFA wameandaa michezo ya kirafiki kwa lengo la kujiimarisha kuelekea mashindano ya CHAN yatakayo anza Agosti 2 , mwaka huu.

Mashindano hayo yatahusisha timu tatu Tanzania, Uganda na Senegali lakini timu zilizotakiwa kushiriki zilikuwa nne mpaka kufikia Jana, ambapo timunya Taifa ya Kenya ilijiondoa na kufanya idadi ya Timu shiriki kusalia tatu, mashindano hayo yatafanyika jijini Arusha.

Kwa mujibu wa ratiba mchezo wa kwanza utapigwa leo Jumanne, Julai 22, ambapo Tanzania itachuana na Uganda, Mchezo wa pili utawakutanisha Uganda na Senegal siku ya Alhamisi, Julai 24, na kisha Jumapili, Julai 27, Tanzania itahitimisha mechi hizo kwa kuvaana na Senegal.

Michezo hiyo mitatu ya kirafiki inalenga kuongeza uimara wa timu hizo kuelekea mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), ambayo huhusisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani pekee.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments