Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Azam FC imekamilisha rasmi usajili wa mlinda mlango wa Taifa Stars, Aishi Manula, akitokea Simba SC, kujiunga kwa mkataba wa miaka mitatu unaomfanya abaki kwenye kikosi hicho hadi mwaka 2028.
Manula, aliyejulikana kama Tanzania one, mmoja wa magolikipa bora wa Tanzania, alianza safari yake Azam FC mapema katika miaka ya 2012–2017 kabla ya kuhamia Simba SC, ambako alirejea na kuijitengenezea heshima na jina ,Taarifa zinaonyesha kuwa sasa amerudi Chamazi, akitarajiwa kuongeza nguvu na uzoefu kwenye milingoti ya Azam fc .
Manula ni golikipa Bora wa kiTanzania ambaye amefanya vizuri kwenye mashindano ya ndani na nje ya Tanzania kwa ngazi ya Klabu mpaka timu ya Taifa , anatarajiwa kurejesha kiwango chake baada ya kukaa benchi kwenye timu Simba na nibaada ya kuruhusu bao Tano dhidi ya Yanga.
Azam fc wanazidi kuimarisha kikosi chao kwa kusajili wachezaji wenye uzoefu na ushindani wa kimataifa, hii sio mara ya kwanza kwa Azam kufanya kusajili mzito kama huu wamefanya mara kadhaa lakini haikuwalipa je, kwa usajili wa mwaka huu Azam fc watafanukiwa Kutwaa kikombe chochote au kufanya vizuri kimataifa ni suala la kusubiri.
0767915473.
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment