MANCHESTER UNITED YAMSJILI BRYAN MBEUMO KUTOKA BRENTFORD

 


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Manchester United imefanikiwa kumsajili kiungo mahiri raia wa Cameroon, Bryan Mbeumo, kutoka Brentford kwa ada ya uhamisho inayofikia pauni milioni 71, ikiwa ni pamoja na bonasi ya pauni milioni 6.

Mbeumo, alifanya vipimo vya afya na alitimiza hatua zote muhimu na kusaini mkataba wa kujiunga rasmi na Mashetani Wekundu, Mkataba wake unatarajiwa kudumu hadi mwezi Juni mwaka 2030, huku kukiwa na chaguo la kuongeza hadi mwaka 2031.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka klabu hiyo, usajili huo unahitimisha jitihada za muda mrefu za United kumsaka kiungo huyo mwenye kasi, ubunifu na uwezo mkubwa wa kupachika mabao katika mashindano mbalimbali.

Kwenye msimu wa 2024/25 Mbeumo alifanya vizuri akiwa na Brentford kwa kuwa na takwimu bora, akicheza michezo 38 nakufunga Jumla ya mabao 20 , akiwa na pasi za usaidizi 8, ukiachana na takwimu hizo licha ya kucheza nafasi ya kiungo lakini alitunza nidhamu yake kwa kupata kadi tatu za njano kwa msimu mzma

Usajili wa Mbeumo ni ishara ya Manchester United kuendelea kujenga kikosi imara chini ya kocha mpya, ikiwa na lengo la kurejea kwenye ushindani wa juu katika Ligi Kuu ya England na michuano ya Ulaya.

Mashabiki wa United duniani kote wameonyesha furaha kubwa kupitia mitandao ya kijamii, wakimtakia heri nyota huyo mpya wa kikosi chao.


0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments