Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Katika kile kinachoonekana kuwa mabadiliko makubwa ya sheria za soka, Bodi ya Kimataifa ya Kusimamia Sheria za Mpira wa Miguu (IFAB) kwa ushirikiano na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), imetoa pendekezo la kufuta kabisa nafasi ya "rebound" kwenye mikwaju ya penati.
IFAB imependekeza kuwa kuanzia Kombe la Dunia 2026, endapo mchezaji atakosa kufunga penati iwe kipa ameokoa au mpira kugonga mwamba basi mchezo usiendelee kama ilivyo sasa, bali utasitishwa mara moja na kipa kuanza upya kwa goal-kick, Hii ina maana kuwa wachezaji hawataruhusiwa tena kufuatilia mpira wa penati kwa nia ya kufunga tena kupitia rebound.
NINI SABABU YA MABADILIKO?
1. Penati zimeonekana kuwa na faida kubwa kwa wapigaji, na hivyo rebound inawaongezea nafasi isiyo ya haki.
2. Kuondoa rebound kutapunguza matatizo ya "encroachment" yaani, wachezaji kuingia eneo la penati kabla ya wakati.
3. Mabadiliko haya yanalenga kuweka uwiano wa haki kati ya wapigaji penati na walinda mlango.
4. IFAB inataka kuhakikisha usawa na ufanisi zaidi katika matumizi ya VAR kwa kuondoa mazingira tata.
MAJARIBIO YATAFANYIKA KABLA 2016
Pendekezo hilo linatarajiwa kuwasilishwa rasmi kwa mkutano mkuu wa IFAB mwezi Februari 2026, Kama litapitishwa, litaanza kufanyiwa majaribio kwenye baadhi ya mashindano maalumu kabla ya kutumika rasmi kwenye Kombe la Dunia.
Hii ni miongoni mwa sheria mpya zinazopendekezwa sambamba na matumizi ya VAR kwenye kadi za njano, na mabadiliko ya namna ya kupiga kona.
Mashabiki wengi duniani wamepokea habari hii kwa hisia tofauti, huku wengine wakiona ni hatua sahihi kulinda haki ya mchezo, ilhali baadhi wakihofia kwamba inaua ladha ya ushindani wa penati.
0767915473.
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment