KOUMA, CHIKOLA NI MALI YA WANANCHI

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Yanga Africans imekamilisha usajili wa wachezaji wawili Lassine Kouma na Often Chikola lengo likiwa ni kuzidi kuimarisha timu hiyo kuelekea msimu ujao wa mashindano.

Kouma ni kiungo mshambuliaji raia wa Mali mwenye umri wa miaka 21 akitokea klabu ya Stade Melien ya nchini Mali , mchezaji huyo anacheza namba 10 , awali alifanya mazungumzo na klabu ya Simba lakini baada ya kuulizia kuhusu soka la Tanzani kwa raia mwenzake golikipa wa Yanga Diarra upepo ulibadilika kwa ushawishi aliopatiwa na mchezaji huyo , na mwisho injinia akamuita kijana na kusaini kandarasi sasa kouma ni mwananchi.

Katika hatua nyingine klabu hiyo imefanikiwa kuinasa saini ya mchezaji mzawa kutokea Tabora united Often Chikola mwenye umri wa miaka (26) mshambuliaji huyo alifanya vizuri msimu uliopita akipachika jumla ya goli (8), na ikumbukwe msimu uliopita katika mchezo ulio wakutanisha Tabora na Yanga , Chikola alifanya vizuri kwa kiwango bora huku akipachika bao kwenye ushindi wa 3-1 dhidi ya waajili wake wa sasa.

 Kwa mujibu ya mashabiki na wadau wa soka nchini wachezaji hao wanahitajika kufanya juhudi za hali ya juu ili kushindana na wachezaji waliopo kwenye kikosi hicho kama vile Max , Mudathiri na Pacome wachezaji ambao wanafanya vizuri katika klabu hiyo, na usajili huu ni mwendelezo wa klabu katika kujenga timu imara kuelekea msimu ujao wa mashindano.

0767915473.

Lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments