KIMYA KIMYA, DIAW KUSAINI SIMBA SC

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Simba SC ipo mbioni kukamilisha usajili wa beki wa kushoto kutoka klabu ya Al Hilal, raia wa Mauritania, Khadim Diaw mwenye umri wa miaka (27), ambaye anatarajiwa kuja kuziba pengo lililoachwa na Zimbwe Jr aliyeondoka hivi karibuni.

Tayali beki huyo ameinza safari ya kuja nchini kwaajili kukamilisha usajili wake na klabu ya Simba, hata hivyo mchezaji huyo ameonyesha kuridhishwa na project inayofanya na klabu hiyo na tayali amekubali kuwa sehemu ya mchakato huo kuelekea msimu ujao wa mashindano.

Usajili wa Khadim Diaw utakuwa sehemu muhimu ya maboresho ya kikosi cha Simba kuelekea msimu mpya wa mashindano ya Ligi Kuu ya NBC na mashindano ya kimataifa, hasa ikizingatiwa kuwa nafasi ya beki wa kushoto ilikuwa imebaki wazi tangu kuondoka kwa Zimbwe Jr

Endapo dili hilo litakamilika, Simba itakuwa imeongeza nguvu mpya katika safu ya ulinzi, huku ikielezwa kuwa uongozi wa klabu hiyo upo makini kuhakikisha wanapata wachezaji wenye uwezo mkubwa na uzoefu wa kimataifa, na safari hii wameahidi kufanya usajili kwa istadi bila mbwe mbwe ila matokea yataonekana uwanjani.

Mashabiki wa Simba wanatarajia kwa hamu kuona mabadiliko hayo yakitimiza matarajio yao ya kutwaa mataji ndani na nje ya nchi msimu ujao, baada ya msimu Jana kuisha bila Kutwaa taji lolote. Je ,usajili wa mwaka huu ambao hauna makele utawalipa Wana lunyasi? ni jambo la muda.


0767915473.

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments