Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mshambuliaji wa Simba SC, Kibu Denis mwenye umri wa miaka (26), anatarajiwa kuwasili Tanzania leo jioni kwa ajili ya kujiunga na kikosi chake ambacho kinajiandaa kuelekea kambini nchini Misri kwa maandalizi ya msimu mpya wa ligi.
Nyota huyo wa Simba alikuwa nchini Marekani kwa ajili ya majaribio katika klabu ya Nashville SC, na sasa anarudi nyumbani baada ya kukamilisha programu hiyo ya majaribio iliyo chukuwa takribani wiki nne za uangalizi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu, Nashville SC wameelekeza Kibu kurejea Tanzania wakati wao wakiendelea kuchambua mwenendo na kiwango alichoonesha katika kipindi cha majaribio, Endapo watariridhisha na uwezo wake, klabu hiyo ya Marekani huenda ikatuma ofa rasmi kwa Simba kwa lengo la kumsajili mchezaji huyo.
Iwapo Nashville wapakabali kiwango Cha kibu na kutumia ofa klabuni hapo timu ya Simba kwanza watapata faida kifedha kwa kumuuza mchezaji huyo, pia kibu atakuwa amefanikisha ndoto yake ya anayoiota ya kukaa karibu na familia yake nchini Marekani.
Kibu ataungana timu ya Simba kuelekea nchini misri kwaajili ya kambi ya maandalizi kwa msimu ujao wa mashindano, kinachosubiriwa ni majibu tu kutoka nchini Marekani kama akishindwa kufuzu majaribio basi ataendelea kusalia msimbazi.
Simba SC kwa sasa ipo katika maandalizi makali kuelekea msimu mpya, na ujio wa Kibu utakuwa chachu katika safu ya ushambuliaji ya timu ambapo kwa msimu huu Timu imemsajili wachezaji wenye uwezo hivyo kibu ataongeza nguvu zaidi kama atasalia klabuni hapo.
0767915473.
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment