Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Katika ulimwengu wa michezo ya ushindani, maandalizi ya mwili na akili hupewa uzito mkubwa. Hata hivyo, suala moja limeendelea kuibua maswali na mijadala miongoni mwa wachezaji, makocha na mashabiki je, ni sahihi kwa mchezaji kufanya mapenzi siku chache kabla ya mchezo muhimu?
Kwa miaka mingi, mada hii imezungumzwa kwa sauti ya chini kana kwamba ni mwiko, lakini sasa wataalamu wa afya na michezo wameamua kulivalia njuga kwa kutoa maoni ya kitaalamu yanayojikita katika utafiti na uzoefu wa wachezaji wa kimataifa.
Kwa mujibu wa Dkt. Benjamin Wema, mtaalamu wa afya ya wanamichezo, hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaothibitisha kuwa tendo la ndoa siku kadhaa kabla ya mchezo linaathiri uwezo wa mchezaji uwanjani.
Aidha, wataalamu wanatahadharisha kuwa mapenzi yanapofanywa muda mfupi kabla ya mchezo, yanaweza kusababisha uchovu wa mwili, kupungua kwa nguvu na kuathiri umakini wa mchezaji uwanjani.
WACHEZAJI WENYEWE WANASEMAJE?
Wachezaji wengi wakongwe na wa sasa wamekuwa wakizungumza kuhusu suala hili kwa nyakati tofauti:
Muhammad Ali, bondia nguli wa Marekani, aliwahi kueleza kuwa alikuwa anajizuia kufanya mapenzi wiki nyingi kabla ya pambano ili asiathirike kimwili, Hali iliyo mfanya awe mahiri ulingoni na kushinda mapambano mengi.
Kwa upande mwingine, baadhi ya wanasoka wa kisasa kama Cristiano Ronaldo wanajulikana kwa nidhamu ya hali ya juu, lakini hawajawahi kuthibitisha kama wanajizuia au la wakisisitiza zaidi juu ya kulinda ratiba na afya ya mwili.
Imekuwa tofauti kwa Diego Maladona ( marehemu kwa sasa) yeye kufanya mapenzi siku chache kabla ya mchezo hakuku muathiri kabisa bali kulimuongezea ubora pindi alipokuwa uwanjani alinukuliwa wakati wa uchezaji wake.
Kitaalam siku chache kabla ya mchezo mchezaji haitakiwi kufanya mapenzi kwa muda mrefu Kwa sababu itamfanya apate uchovu lakini akifanya mapenzi kwa muda mfupi inaweza kufanya kujihisi mwepesi na mwenye furaha na akafanya vizuri. Hivyo athari hupatikana kutokana na mtu mwenyewe.
0767915473.
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment