Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mshambuliaji wa Newcastle United, Alexander Isak, ameripotiwa kuendelea kusubiri kwa matumaini makubwa kujiunga na klabu ya Liverpool, akisisitiza kuwa hiyo ndiyo timu pekee anayopendelea kuchezea kwa msimu huu wa usajili.
Taarifa zinaeleza kuwa Isak hajaungana na wenzake kwenye mazoezi ya timu wiki hii, huku akitajwa kuwa hana nia ya kujiunga na klabu ya Al Hilal kama ilivyodaiwa awali madai ambayo yamekanushwa vikali.
Inaelezwa kuwa tayari Isak alifikia makubaliano binafsi na Liverpool wiki kadhaa zilizopita, jambo linaloashiria kuwa mazungumzo ya upande wake hayana kikwazo, bali hatua inayosubiriwa kwa sasa ni kutoka kwa Newcastle endapo wataamua kumruhusu.
Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na mchezaji huyo, Liverpool wako tayari kutoa dau kubwa zaidi kuwahi kutolewa katika historia ya klabu hiyo ili kumnasa Isak, lakini maamuzi yote yapo mikononi mwa Newcastle.
Ikumbukwe awali Isak alikuwa anafuatiliwa kwa katibu na Liverpool lakini kuchelewa kwa maridhiano baina Yao ulifanya Liverpool kubadilisha upepo na kugonga hodi mpaka Frankfurt na kumsajili Ekitike , sasa Isak kaonyesha Yuko tayali na kinachosubiriwa ni mchezaji huyo kufikia makubaliano ya pamoja.
Endapo Newcastle watakubali ofa hiyo, huenda Isak akatua rasmi Anfield katika siku chache zijazo, jambo ambalo linaweza kuongeza nguvu mpya kwenye kikosi cha kocha mpya wa Liverpool msimu ujao.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment