IBENGE AGEUKA KIKWAZO SIMBA KUMNASA FEI

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kocha mpya wa klabu ya Azam FC, Florent Ibenge, ametoa msimamo mkali kwa uongozi wa klabu hiyo akiwataka wasimuuze kiungo wake tegemeo, Feisal Salum maarufu kama Fei Toto, katika dirisha hili la usajili.

Taarifa zinaeleza kuwa Ibenge ameweka wazi kuwa hawezi kumruhusu mchezaji huyo kuondoka kwa gharama yoyote ile, akisisitiza kuwa anapanga kujenga kikosi chake kipya kwa kutetemea huduma ya mchezaji huyo, yaani timu ya Azam icheze kwa kumzunguka Feisal hivyo hayupo tayali kuona mchezaji huyo anaondoka na ameuomba uongozi wa timu hiyo kutumia gharama yoyote mchezaji huyo abakie klabuni hapo.

Ingawa klabu ya Simba SC imekuwa katika mazungumzo ya muda mrefu na viongozi wa Azam FC kwa lengo la kunasa Saini ya Fei Toto, lakini bado hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa hadi sasa, huku Kocha Ibenge akiripotiwa kugoma kabisa kuidhinisha uhamisho huo, lakini Simba wakiendelea kuwa na matumaini ya kuipata saini ya nyota huyo.

Fei Toto, ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake na Azam FC, anaweza kuwa mchezaji huru mwakani endapo Azam FC haitafanikiwa kumbakisha kabla ya mwezi Juni mwaka 2026.

Licha la kocha huyo kutia ngumu lakini bado klabu ya Simba inahakikisha kuwa inapambana kupata Saini ya Fei Toto na jitihada bado hazijafikia tamati na suala na mchezaji huyo kujiunga Simba au kusalia Azam ni hamsini kwa hamsini.

Hatua hii ya Ibenge inaonesha dhamira yake ya kuijenga Azam FC upya kwa kuwatumia wachezaji wenye ubora wa hali ya juu, huku Simba wakilazimika kutafuta njia nyingine iwapo ndoto zao za kumsajili Fei Toto zitazimwa rasmi.


0767915473

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments