HALMASHAURI YA JIJI YAIKALIA KOONI FC BARCELONA

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya soka ya FC Barcelona imekumbwa na pigo kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa mashindano baada ya halmashauri ya Jiji la Barcelona kukataa kutoa lesseni kwaajili ya kuruhusu uwanja wa Spotify camp Nou kutumia kwenye michezo ya klabu hiyo.

 hatua hiyo imetokana na kuchelewa kwa ukamilishaji wa baadhi ya kazi muhimu kwenye uwanja huo, zikiwemo sehemu za VIP, paa, mifumo ya umeme na ulinzi, pamoja na mazingira ya nje ya uwanja, Kutokana na hali hiyo, Barcelona haijapata kibali rasmi cha matumizi kutoka kwa halmashauri ya jiji, jambo linalowazuia kupokea mashabiki au kuandaa mechi yoyote rasmi.

Mwezi uliopita Barcelona ilitangaza nia ya kurudi uwanjanwao wa nyumbani Spotify camp Nou kwaajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Como ambao umepangwa Kupigwa Agosti 10, lakini mipango huo hautatekelezwa Hadi pale matengenezo ya uwanja yatakapo kamilika na halmashauri kutoa kibali kwaajili ya shughuli za michezo.

Mashabiki wa Barcelona pamoja na viongozi wa klabu hiyo wameonesha masikitiko yao kutokana na hali hiyo, hasa ikizingatiwa kuwa uwanja huo ulitarajiwa kufunguliwa upya kwa heshima ya nyota wao wa zamani Lionel Messi, ambaye pia angeweza kuheshimiwa kupitia mchezo wa Gamper mwaka huu.

Kwa sasa, klabu hiyo inasubiri maamuzi ya mwisho kutoka kwa halmashauri ya jiji, huku ikilazimika kuandaa mipango mbadala kwa ajili ya michezo ya mwanzo.



0767915473.

lugembetimothy01@gmail.com.

0/Post a Comment/Comments