Mwanakwetusports.
Klabu ya Liverpool imekamilisha usajili wa mshambuliaji chipukizi kutoka Entrach Frankfurt raia wa Ufaransa, Hugo Ekitike (22), baada ya kufuzu vipimo vya afya na kukubali masharti ya mkataba wake mpya na klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England.
Kupitia kurasa zao rasmi, Liverpool FC wamethibitisha ujio wa Ekitike ambaye amekuwa akihusishwa na klabu hiyo kwa kipindi kirefu, Mchezaji huyo pia alithibitisha taarifa hizo kupitia akaunti yake binafsi, akionyesha furaha na shukrani kwa kupata nafasi ya kujiunga na moja ya klabu kubwa zaidi barani Ulaya.
Liverpool imelipa ada ya €80 milioni kama malipo ya moja kwa moja, huku ikiwa na vipengele vya nyongeza vinavyoweza kuongeza thamani ya mkataba huo hadi kufikia €95 milioni, Nyongeza hizo ni pamoja na €10 milioni kama bonasi rahisi ambazo ni rahisi kutimizwa kulingana na vigezo vya kawaida kama idadi ya mechi au mabao, na €5 milioni nyingine kama bonasi ngumu, ambazo zinaweza kujumuisha mafanikio makubwa kama kushinda mataji ya ligi au Ulaya.
Ekitike, ambaye amekuwa akicheza soka la kiwango cha juu barani Ulaya akiwa na klabu ya Frankfurt , anakuja Liverpool katika kipindi ambacho kocha Arne Slot anatafuta kuimarisha safu ya ushambuliaji, Ujio wake unaongeza ushindani mbele pamoja na washambuliaji kama Darwin Nunez, na Mohamed Salah.
Na rasmi klabu imempatia Ekitike jezi namba (54) kwa muda kwa kipindi Cha michezo ya maandalizi kuelekea kuuanza msimu mpya wa ligi.
Mashabiki wa Liverpool wamelipokea kwa furaha taarifa hii, wakitazamia kuona kiwango cha mshambuliaji huyo mwenye kasi, uwezo wa kumalizia, na kufunga mabao.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment