CHUMA KUTOKA MAMELODI NDANI YA SIMBA MWAKA MMOJA

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Simba SC imekamilisha usajili wa beki wa kati kutoka Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Rushine De Reuck, mwenye umri wa miaka 29, kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Beki huyo msimu uliopita alitumikia klabu ya Maccabi Petah Tikva ya Israel kwa mkopo, ameshiriki jumla ya michezo minne pekee katika awamu ya pili ya msimu, Usajili huu unakuja ikiwa ni baada ya De Reuck kuhitimisha huduma yake ya miaka minne ndani ya kikosi cha Sundowns, na kushindwa kuendeleza huduma yake katika kikosi hicho.

Rushine alijiunga na Mamelodi Sundowns mwaka 2021 akitokea Maritzburg United, akiwa ametangazwa kuwa Beki Bora wa Msimu wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini, Akiwa Maritzburg, alikuwa akifanya kazi chini ya Kocha Mkuu wa sasa wa Simba SC, Fadlu Davids hali inayozidisha imani juu ya mchango wake ndani ya kikosi hicho cha Msimbazi, kwakuwa kocha mwenyewe anaonekana anamfahamu vyema mchezaji huyo.

Mashabiki wa Simba kwa muda wallikuwa wakiiomba klabu hiyo kuongeza beki wa kati atakaye saidiana na Kagoma kwenye majukumu ya kiulinzi ya timu hiyo hatimaye kilio chao kimesikika na rasmi kiungo wa kati Rushine atasaidiana na Kagoma.

Ujio wa De Reuck unatazamwa kama hatua madhubuti ya Simba SC katika kuimarisha safu yao ya ulinzi kuelekea msimu mpya wa mashindano ya ndani na kimataifa, Mashabiki wa Simba wanatarajia kuona mchango mkubwa kutoka kwa beki huyo mwenye uzoefu mkubwa barani Afrika.


0767915473.

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments