Timothy Lugembe,
0767915473
Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 2 Agosti mwaka huu, yakifanyika kwa mara ya kwanza katika nchi tatu kwa pamoja , Tanzania, Kenya na Uganda, hii ni fursa adhimu kwa ukanda wa Afrika Mashariki, si tu katika kukuza vipaji vya michezo, bali pia katika sekta ya biashara na uchumi kwa ujumla.
Tayari maandalizi yanaendelea kwa kasi kubwa katika nchi hizo, huku miundombinu ya viwanja, hoteli na huduma nyingine za kijamii ikiwekwa sawa kupokea wageni kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, CHAN ni fursa ya kiuchumi hasa kwa wafanyabiashara wadogo na katika sekta ya utalii pamoja na Hoteli.
Wataalamu wa uchumi na michezo wanakubaliana kuwa tukio hili linatarajiwa kuongeza mzunguko wa fedha kupitia shughuli mbali mbali kama vile.
-Mauzo ya bidhaa za kumbukumbu (vitenge, bendera, jezi na mapambo ya asili kama vile vinyago )
-Huduma za malazi na chakula, hapa wafanyabiashara wa Hotelini na migahawani wamepata fursa kwani idadi ya watu watakao kuwa wakielekea uwanjani watahitaji kula pia kulala hivyo ni fursa ya kuingiza kipato
-Usafirishaji na utalii wa ndani, vyombo vya usafiri kama vile boda boda , bajaji na magari watanufaika kutokana na mzunguko wa watu kuelekea na nakutoka viwanjani.
-Matangazo ya biashara kupitia televisheni na majukwaa ya kidijitali, hapa mahoteli na nyumba za wageni watatumia fursa ya kutengeneza Matangazo ya biashara kwenye vyombo vya habari na kutengeneza faida kifedha kwa vyombo hivyo.
-Ajira za muda kwa vijana katika maeneo ya michezo, hapa Kuna kufanya usafi maeneo ya viwanja pia kwa ball boys hii ni fursa
-Fursa kwa wasanii wa ndani kupitia burudani mbalimbali zitakazoambatana na mashindano wasanii kutoka katika nchi hizo watapata jukwaa la kutumbuiza na kutambulika kimataifa na kuongeza Mashabiki katika kazi zao.
Huu ni mwanzo tu wananchi na wafanya biashara wakubwa na wadogo wajiandae zaidi kwani huu ni mwanzo tu pia Kuna mashindano makubwa zaidi yatafanyika katika nchi hizo baada ya haya , ambayo ni AFCON, serikali zimeshatengeneza miundo mbinu ipo sawa Sasa ni zamu ya wafanyabiashara na wananchi wengine kuhakikisha fursa hii haipiti hivi hivi.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment