Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kiungo nyota wa Yanga SC, Stephane Aziz Ki, anatarajiwa kurejea kambini Jangwani kabla ya Julai 10, 2025, baada ya mkataba wake wa mkopo na Wydad Casablanca wa Morocco kukamilika rasmi.
Aziz Ki alijiunga na Wydad kwa mkopo wa muda wa miezi miwili, akiwasaidia katika kampeni ya Kombe la Dunia la Klabu (FIFA Club World Cup), Mkataba huo ulijumuisha kipengele cha ununuzi wa moja kwa moja kwa ada ya Sh1.7 bilioni, lakini hadi sasa Wydad haijaonyesha nia ya kumchukua moja kwa moja.
Habari kutoka vyanzo vya ndani ya klabu ya Wydad zinaeleza kuwa kocha wa timu hiyo amependekeza nyota huyo arejee Yanga ili kupisha nafasi kwa sajili mpya katika dirisha la usajili linaloendelea.
Kwa mujibu wa makubaliano ya awali, iwapo Wydad haitatumia kipengele cha kumnunua Aziz, italazimika kulipa kiasi cha dola 150,000 (takriban Sh395 milioni) kwa Yanga kama fidia ya mkopo wa miezi miwili.
Aziz, ambaye mchango wake ulionekana kuwa wa muhimu kwa Wydad katika mashindano ya kimataifa, sasa Kuna uwezekano akarudi Tanzania kuendelea na majukumu yake ya kikosi cha Yanga kwa msimu mpya unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Kurejea kwa Azzi Ki , kutaenda kuimarisha kikosi Cha wananchi kuelekea mashindano mbali mbali yanayotarajiwa kufanyika hasa hasa ligi ya mabingwa Afrika.
0767815473.
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment