YOUNG AFRICANS WAMEWEKA MISIMAMO THABITI DHIDI YA MICHEZO ILIYOBAKI

 

Na Timothy Lugembe 

Klabu ya Yanga SC imetoa tamko kupitia msemaji wake Ally Kamwe kuwa hawatahudhuria mechi tatu zilizosalia msimu huu wa Ligi Kuu Bara pamoja na fainali ya Kombe la Shirikisho hadi masharti yao ya kikatiba yatakapotimizwa rasmi na vyama vinavyosimamia soka, yaani TPLB na TFF .

Yanga wanasema TFF hawajalipa fedha ya mashindano ya Kombe la Shirikisho msimu uliopita hali inayofanya wasusie kushiri fainali ya shirikisho msimu huu mpaka pale watakapo pewa fedha zao za malipo ambapo mdhamini wa mashindano hayo benki ya CRDB imekiri kulipia fedha hizo kwa TFF.

Mpango wa CRDB Bank yenyewe wamesema walilipia fedha hizo kwa TFF kama sehemu ya zawadi, lakini TFF wanadai Yanga walitaka kiasi hicho kiwekwe kama msingi wa kulipa ada za wachezaji wao wa kimataifa.

Kutokana na msimamo uleule, Yanga wameonya kwamba hawatacheza mchezo wowote hadi malalamiko yao yameratibiwa na kukubaliwa , na walienda mbali zaid ikiwa matakwa Yao hayatosikilizwa msimu ujao watatafuta sehemu nyingine ya kushiriki ligi.



lugembetimothy01@gmail.com

0/Post a Comment/Comments