YANGA WACHUKUA UBINGWA MBELE YA MTANI, WAMSINDIKIZA NA KICHAPO CHA 2-0.

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mchezo wa namba 184 wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya mahasimu wa jadi, Yanga SC na Simba SC, uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, umetamatika kwa kishindo huku Yanga wakiandika historia nyingine kwa kutwaa ubingwa wa msimu wa 2024/2025 mbele ya watani wao wa jadi kwa ushindi wa mabao 2-0.

Katika pambano hilo lililovuta hisia za mashabiki kote nchini, Yanga walionekana kuwa bora zaidi, wakitawala mchezo kipindi chote na kupeleka kilio Msimbazi, Bao la kwanza lilifungwa dakika ya 67 kupitia mkwaju wa penalti uliopigwa na nyota wa Ivory Coast, Pacome Zouzoua, baada ya kipa wa Simba, Pinpin Camara, kumchezea madhambi ndani ya eneo la hatari.

Dakika ya 88, mashambulizi makali ya Yanga yalizaa matunda tena baada ya Clement Mzize kupokea pasi safi kutoka kwa Zouzoua na kuunganisha kwa ustadi wavuni, akiwachanganya mabeki wa Simba na kuua mchezo.

Kwa mara ya tano mfululizo, Simba wanakumbana na kichapo mikononi mwa Yanga katika michezo ya watani wa jadi, huku wakiwa hawajashinda taji lolote la Ligi Kuu kwa misimu minne sasa hali inayoonesha dhahiri kwamba wameporomoka na Yanga wanaendelea kutawala.

Kwa ushindi huo, Yanga wanafikisha mataji 30 ya Ligi Kuu, wakizidiwa mataji 8 tu na Simba waliopo na vikombe 22. Hali hii inaifanya Yanga kuonekana imara zaidi kisoka kwa sasa, hasa kwenye mechi kubwa.

Kocha wa Simba Fadlu Davis amewapongeza Yanga na kusifu ubora wa kikosi chao kwa kuwa na wachezaji wenye hari ya kupambana na uzoefu kwenye michezo mikubwa, ameongeza kuwa licha ya mambo kwenda ndivyobsivyo lakini wamevuka malengo licha ya kikosi walicho nacho na akipo ulizwa kuhusu mustakabali wake klabuni hapo alijibu tutaona.

Kocha wa Yanga Miloud Hamdi amewashukuru wachezaji, Mashabiki na viongozi kwa kuwa nae bega kwa bega Hadi kufikia mafanikio hayo na amewashukuru Tena wachezaji kwa kufuata walicho wa elekeza na kuibuka na ushindi huo.

Baada ya ligi kutamatika sasa kinacho subiriwa ni tuzo kuona nani nani wamefanya vizuri huku Kuna baadhi ya tuzo zikiwa tayali Zina pakwenda mfano Mfungaji Bora ni Jean Ahoua kutoka Simba , kipa Bora Pinpin Camara kutoka Simba, kocha Bora anatarajiwa kuwa Fadlu Davis kutokana na takwimu zinambeba zaidi huku tuzo nyingine zikisubiri uamuzi wa shirikisho.



0767915473.

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments