Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Yanga SC imemuwekea pingamizi Rais wa TFF Wallace Karia na pingamizi hilo limewasilishwa ofisi za TFF likiwa limesainiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wao (CEO) Andre Ntine.
Yanga SC katika pingamizi lao wanaitaka Kamati ya Uchaguzi chini ya Mwenyekiti wake Wakili Kilomoni Kibamba kumuondoa Karia katika kinyang'anyiro cha Uchaguzi wakiwa na hoja Kuu 3:
1. Matumizi mabaya ya madaraka kwa kuchukua endorsement 46 Kati ya 47
2. Kuanza kampeni kabla ya muda kwa kukusanya endorsement 46 kabla ya tangazo la Uchaguzi kutolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
3. Wanapinga Karia kugombea mara ya 3 wakisema ni kinyume na sera ya michezo nchini ambayo inataka vyama vya michezo viongozi wake kukaa madarakani kwa vipindi 3 vya miaka mitatu mitatu au vipindi 2 vya miaka minne minne.
Kinacho subiriwa ni majibu kutoka kamati ya uchaguzi kuhusu shauri hilo, swali la kujiuliza ni je Wallece karia ikiwa ni kweli Yuko kinyume ataondolewa kwenye kinyang'anyiro??
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment