Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
TImu ya Yanga Africans wameng'ara msimu huu kwenye mashindano ya ndani kwa msimu wa 2024/2025 baada ya kuchukua Kila kikombe wakianza na Ngao ya jamii, Ligi kuu bara, na wamekamilisha kwa kuchukua CRDB FEDERATION kwa kuichapa Singida black stars 2-0 kwenye mchezo uliopigwa Amani Zanzibar.
Katika mchezo huo magoli ya Yanga yalifungwa na Duke Abuya na bao la pili likifungwa na Clement Mzize , mchezo huo ulikuwa ni wakiushindani kwa Timu zote huku Yanga wakionekana kuwa Bora zaidi huku dakika ya 86 Mshambuliaji wa Yanga Jonathan Sowah akionyeshwa kadi nyekundu kutokana na utovu wa nidhamu.
Klabu ya Yanga imekuwa na kiwango ambacho kinamuendelezo kwa miaka minne mfululizo kwa kuchukua makombe ya ligi na federation Cup, huku ikichagizwa zaidi na kumfunga mtani wao Simba sports.
Leo hii June 30, 2025 klabu hiyo unatarajia kufanya Paredi kwenye maneno kadhaa jijini Dar es laam ikiwemo mitaa ya jangwani na msimbazi wakitembeza vikombe walivyo twaa kwa msimu huu .
Mafanikio ya Yanga ni matokeo ya uwekezaji na uongozi imara na ushirikiano wa washabiki na timu yao chini ya uongozi thabiti wa muhandisi Hersi Saidi, kwa sasa msimu umemalizika kinachosubiriwa ni timu kujipanga kwaajili ya msimu mpya.
0767914473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment