Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mchezo wa mzunguko wa pili kati ya Yanga na Simba ambao ulio pelekwa mbele na kutarajiwa kufanyika tarehe 15mwezi huu uwanja wa Benjamin mkapa jijini Dar es salaam umekuwa na viashiria mbali mbali vya kutofanyika tarehe hiyo au kutocheza kabisa.
Viashilia hivyo vimeonekana baada ya msemaji wa Yanga Africans Ally Kamwe kusema kuwa kwa sasa wapo kambimi wakijiandaa na michezo miwili iliyopo mbele Yao ambayo ni dhidi ya Tanzania Prison na Dodoma jiji lakini hakutaja kama wanamchezo dhidi ya Simba siku ya Tarehe 15 hiyo yote nikatika kusimamia msimamo wao kuwa hawachezi derby.
Kiashilia Cha pili kutokana na kanuni kuwa timu mwenyeji inatakiwa kutangaza viingilio vya mchezo huo pia kuweka kikao dhidi timu na kamati ya ulinzi na usalama kama sehemu za maandili kuelekea mchezo husika lakini timu ya Yanga haijafanya hivyo kitu kinacho ashiria kuwa mchezo hautakuwepo.
Mpaka sasa madai ya timu ya Yanga nikuwa hawatacheza mpaka viongozi wa bodi ya ligi watoe sababu zenye mashiko kwanini derby iliyo takiwa kufanyika tarehe 8 mwez 3 mwaka huu haijafanyika ambapo kwa mujibu wao hawajapewa sababu , hizo lakini pia wanahitaji baadhi ya viongozi wa bodi ya ligi wajiuzuru lakini mpaka sasa havija fanyika, ikiwa vitu hivyo vikifanyika wao watacheza ila visipo fanyika hawatacheza mchezo.
0767915473.
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment