Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Timu ya Ukerewe Queens imeibuka mabingwa wa Ligi Daraja la Kwanza Wanawake (WFDL) kwa msimu wa 2024/2025, baada ya kuiadhibu Bilo FC bao 3-0 kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza siku ya 16 June 2025.
Katika fainali, Ukerewe Queens walikutana na Bilo FC ambapo walipata ushindi wa mabao 3-0, na hivyo kuibuka mabingwa rasmi wa WFDL 2024/2025, Ushindi huo uliwapa tiketi ya kupanda daraja na kujiunga na Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) msimu ujao, hatua inayochukuliwa kuwa ni mafanikio makubwa kwa timu hiyo kutoka visiwani Ukerewe mkoani Mwanza.
Sherehe za kukabidhi kombe zilifanyika mbele ya mashabiki, viongozi wa serikali na maafisa wa TFF ambapo timu hiyo ilipongezwa kwa kuonesha dhamira, kujituma na ushindani mkubwa kipindi chote cha ligi.
Mafanikio haya yanatajwa kuwa ni chachu kwa maendeleo ya soka la wanawake nchini huku Ukerewe Queens wakielezwa kuwa mfano wa kuigwa kwa jinsi walivyopambana hadi kufikia mafanikio hayo makubwa.
TFF imetoa pongezi kwa timu hiyo na kuzihimiza timu nyingine kuiga mfano huo katika kukuza vipaji vya wanawake katika soka nchini.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment