Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars, imefanikiwa kutwaa ubingwa wa CECAFA Senior Women’s Championship 2025 baada ya kuichapa Kenya kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa katika uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Kabla ya fainali timu zote zilikuwa hazijafungwa hivyo kufanya mchezo uwe mzuri na wakuvutia , mpaka kipindi Cha kwanza kinakamilika kulikuwa hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzake lakini baadae mapema kipindi Cha pili dakika ya 49' mchezaji wa Kenya Enez Mango alijifunga goli ambalo lilidumu kwa dakika zote tisini na Twiga stars kuibuka mabingwa.
Katika tuzo Twiga stars wametawala huku tuzo ya kipa Bora ikichukuliwa na Naijiati Iddrissa , mchezaji Bora akiwa Diana Lucas, huku mfungaji Bora akiwa oppa Clement hii yote nikutokana na ubora wa kikosi hicho na matunda yameonekana kupitia ubingwa na tuzo mbalimbali.
Soka la wanawake la Tanzania linazidi kukua kwa kasi kutokana na uwekezaji unaozidi kufanywa na TFF kwa kuimarisha ligi na kuzifanya kuwa ya ushindani na matokeo yake ndio haya Tanzania wanazidi kulitawala soka la Africa mashariki na kati.
0767915473.
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment