TPLB: MWENYEKITI AJIUZURU, MTENDAJI MKUU ASIMAMISHWA KAZI

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Katika hatua isiyotarajiwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Steven Mnguto, amejiuzulu rasmi wadhifa wake kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Katibu Mkuu wa TFF, CPSP Kidao Wilfred, barua ya kujiuzulu kwa Mnguto imepokelewa na uongozi wa TFF na hatua hiyo imethibitishwa tarehe 13 Juni 2025

Katika hatua nyingine kubwa, Rais wa TFF, Wallace Karia, amechukua hatua ya kumsimamisha kazi Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPLB, Almasi Kasongo, huku sababu za hatua hiyo zikiwa hazijafafanuliwa wazi katika taarifa hiyo.


Maamuzi hayo yamefanyika kufutia shinikizo kubwa lililofanywa na club ya Yanga baada ya mara kadhaa kuombwa kujiuzurubkwa viongozi hao kwani timu hiyo haikuwa na Imani na viongozi hao na rasmi ombi la wananchi limefanikiwa.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.

0/Post a Comment/Comments