Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Katika miaka ya hivi karibuni, timu kutoka Afrika Kaskazini zimeendelea kuonyesha ubabe na uthabiti mkubwa katika michuano ya vilabu barani Afrika, ikiwemo CAF Champions League na CAF Confederation Cup, Mafanikio haya yamezidi kuthibitisha kuwa ukanda wa Kaskazini ni miongoni mwa vinara wa soka barani Afrika.
Katika michuano ya CAF Champions League, klabu kama Al Ahly ya Misri, Wydad Casablanca ya Morocco, na Esperance de Tunis ya Tunisia zimekuwa zikifikia hatua za juu kila msimu, huku Al Ahly ikiwa kinara wa kihistoria kwa kutwaa taji hilo zaidi ya mara 11. Katika miaka mitano iliyopita, Al Ahly na Wydad wamekutana mara kadhaa katika fainali, jambo linaloonyesha ubora wa timu hizo.
Kwa upande wa CAF Confederation Cup, timu kama RS Berkane ya Morocco, Pyramids FC ya Misri, cs sfaxen ya Algeria na USM Alger ya Algeria zimekuwa na mafanikio makubwa pia. RS Berkane, kwa mfano, wametwaa taji hilo mara kadhaa ndani ya kipindi kifupi, ikiwa ni ishara ya uwekezaji bora na usimamizi wa kisasa.
Kwa mwaka huu Timu kutoka KASKAZINI zimeendelea kuonyesha utawala wao baada ya kuchukua makombe yote yanayo endeshwa shirikisho la mpira Africa , katika mashindano ya klabu bingwa Africa imeshuhudiwa Timu ya Pyramid kutoka nchini Misri ikitwaa ubingwa kwa kuichapa Mamelod sundown ya Africa kusini kwa Jumla ya magoli 3-2, huku kwenye kombe la shirikisho wakitwaa RS Berkane kutoka moroko kwa kuwafunga Simba Sc kutoka Tanzania kwa Jumla ya mabao 3-1.
Hata hivyo Timu za Kanda ya Africa mashabiki na kati tunazungumzia Simba,Yanga, Mamelod sundown, Orlando Pirate na Tp mazembe zinaonyesha kuwa kama zikizidi kuongeaza uwekezaji wataweza kurudisha ushindani dhidi ya Timu za kaskazini.
Hivyo uwekezaji katika miundo mbinu ya viwanja vya kuchezea na kufanyika mazoezi unahitajika kwa virabu vya Kanda nyingine na vijitahidi kuachan kuchanganya mpira na masuala ya siasa .
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment