Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Katika hatua ya kihistoria ya kuongeza uwazi na uwajibikaji katika mchezo wa soka, waamuzi wa kimataifa sasa wameanza kuvaa kamera maalum wakati wa michezo mbalimbali duniani, hatua inayolenga kulinda maamuzi ya waamuzi, kuongeza imani kwa mashabiki, na kusaidia marejeo ya kiufundi.
Teknolojia hii mpya ambayo tayari imeanza kufanyiwa majaribio katika baadhi ya mashindano makubwa barani Ulaya na Amerika, ikiwemo FIFA CLUB WORLD CUP inawawezesha waamuzi kurekodi kila kitu wanachokiona, kusikia na kusema wakiwa uwanjani, Kamera hizo ndogo huwekwa kwenye sare ya waamuzi, hususan kifuani au kwenye miwani maalum ya kisasa.
Kwa mujibu wa maofisa wa FIFA, matumizi ya kamera hizo si tu kwamba yatasaidia katika utatuzi wa migogoro ya maamuzi ya utata, bali pia yatatoa mafunzo kwa waamuzi chipukizi wanaojifunza kupitia video halisi za mechi Pia, mashabiki wataweza kuelewa kwa kina kile kilichokuwa kinaendelea wakati wa tukio husika kama penati, faulo au kadi nyekundu.
Hata hivyo, si wote wanaounga mkono hatua hiyo. Baadhi ya makocha na wachezaji wanasema inaweza kuleta presha kwa waamuzi au kuvunja hali ya kujiamini, huku wengine wakihofia kuhusu faragha ya mawasiliano ya ndani ya mechi,vHata hivyo, mashirikisho mengi yamesema maudhui hayo hayatatumika hadharani bila idhini maalum.
Teknolojia hii inaelezwa kuwa sehemu ya mabadiliko ya kisasa katika soka yanayolenga kuifanya michezo kuwa ya haki, yenye ushindani wa kweli na iliyo wazi kwa wote,vKwa sasa, UEFA tayari wamepanga kutumia kamera hizo kwenye baadhi ya michezo ya hatua za mtoano msimu huu.
Ni wazi kuwa, soka linaingia kwenye zama mpya za uwazi na uwajibikaji zaidi ambapo kila sauti, kila neno na kila hatua ya mwamuzi itakuwa sehemu ya kumbukumbu ya mchezo.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment