Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Hemed Suleiman "Morocco", amesema kuwa maandalizi ya timu yake kuelekea mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) utakao fanyika Tarehe 6-mwezi wa 6 mwaka huu polokwane nchini Africa kusini yanaendelea vizuri.
Akizungumza katika kambi ya timu hiyo, kocha Morocco alieleza kuwa hakuna mchezaji majeruhi kwenye kikosi hicho hadi sasa, na wachezaji wote wanaendelea na mazoezi kwa hari morali ya hali ya juu.
Amesema kuwa kila mchezaji anaonyesha utayari wa kuisaidia timu, jambo linalompa moyo mkubwa kuelekea mchezo huo muhimu. Aidha, Morocco amesema kuwa mechi dhidi ya Bafana Bafana ni nafasi nzuri kwa timu yake kujiandaa vyema kuelekea michuano ya CHAN, ambayo hujumuisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani pekee.
Kwa upande wake, mchezaji wa Taifa Stars, Mirajy Abdallah, amesema kuwa maandalizi ya timu yako vizuri na wanazingatia kila maelekezo kutoka kwa benchi la ufundi. Mirajy amesema kuwa ni furaha kubwa kwake kurejea kwenye kikosi cha Taifa na kuona anapewa nafasi tena kuitumikia timu hiyo.
0767915473
lugembetimothy01@gmail.com.
Post a Comment