SIRI YA MCHEZAJI BORA WA MCHEZO HII HAPA


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Katika ulimwengu wa soka, wengi bado wamefungwa na dhana ya kwamba kufunga bao ndiyo kipimo kikuu cha ubora wa mchezaji, Lakini kwa mujibu wa wachambuzi wa soka ukweli ni tofauti kabisa, inawezekana kabisa mchezaji afunge bao lakini bado asiwe Mchezaji Bora wa Mechi (MAN OF THE MATCH) kama mchango wake kwa timu kwa ujumla ulikuwa mdogo.

Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali vya soka , kuna vigezo vingine vya msingi vinavyozingatiwa katika kumpata nyota wa mechi, Miongoni mwao ni asilimia ya pasi sahihi (pass completion), ufanisi wa kuzuia mashambulizi (tackle success), na usahihi wa mashuti langoni (shooting accuracy), mchezaji anayehakikisha pasi zake zinafika kwa walengwa, anayerejesha umiliki wa mpira kwa timu yake, na anayepiga mashuti yaliyo na lengo sahihi, ana nafasi kubwa ya kuibuka nyota wa mchezo.

Kwa upande wa makipa, suala haliegemei tu kwenye kuokoa mipira, Watazamaji makini huangalia pia namna kipa anavyosoma mchezo, anavyotoa maelekezo kwa safu ya ulinzi, na hata ubora wa pasi zake kuelekea mbele, Hii ina maana kuwa hata kama kipa amefanya 'saves' 50" lakini akaruhusu bao muhimu au akawa chanzo cha upungufu wa nidhamu ya safu ya ulinzi, huenda asipewe heshima hiyo ya (MAN OF THE MATCH).

Pia wachezaji wanaoamua mechi kwa hatua moja muhimu kama kutoa pasi ya bao (assist), kuzuia bao la wazi, au hata kuamsha morali ya timu nao wana nafasi ya kuonekana mashujaa wa siku, Ni wazi kwamba soka si mchezo wa takwimu za kufunga pekee, bali ni mchanganyiko wa mbinu, akili, nidhamu, na mchango wa pamoja.

Kwa hiyo, wakati mwingine unaweza kushangaa kwanini mfungaji hakutajwa kama nyota wa mechi, Jibu liko hapa, kuna waliovuja jasho kisirisiri, wakavuruga mipango ya wapinzani, wakafanya kazi isiyoonekana lakini yenye matokeo makubwa, Hawa ndio mashujaa wa kweli wa dakika 90 na soka limeanza kuwaenzi ipasavyo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.

0/Post a Comment/Comments